TAHLISO yatoa wiki moja kwa serikali kutoa mikopo
Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa.