Vincent Bossou
Bossou amesema, mazoezi ya Lwandamina, yamekuwa na utofauti mkubwa na mtangulizi wake Mholanzi, Hans Van der Pluijm, ambaye ndiye aliyemsajili kwenye kikosi hicho akitokea kwao Togo mwanzoni mwa msimu uliopita.
Beki huyo amesema anafurahi kuona hamasa ya wachezaji imeongezeka ndani ya timu na kila mmoja anafanya mazoezi kwa bidii, kitu ambacho kinampa matumaini ya kuweza kutetea ubingwa wao wakiwa chini ya kocha huyo mpya.
“Tumebakiza pointi mbili dhidi ya Simba, ili tuongoza ligi, ni jambo gumu lakini linawezekana kutokana na kasi tuliyokuwa nayo hivi sasa kila mchezaji anataka kucheza kwa bidii ili kutafuta nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza,” amesema Bossou.




