Hatuko tayari kuuza magogo nje ya nchi - Maghembe
Waziri wa Maliasili na utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amesema Tanzania haiko tayari kuuza magogo nje ya nchi na badala yake shughuli za kuvuna magogo hayo zitafanyika hapa nchini ili kuchochea uanzishwaji wa viwanda na ajira kwa wananchi wake.