Watumishi TRA wafikishwa mahakamani kwa rushwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU imewafikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, maafisa wawili pamoja na kibarua mmoja wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kwa makosa matatu ya kuomba na kupokea rushwa.

