Wahandisi wataka awepo Mhandisi Mkuu wa Serikali
Taasisi ya wahandisi Tanzania imeiomba serikali kuweka Mhadisi Mkuu wa Serikali ambaye ataratibu na kusimamia sekta zote za uhandisi nchini ili kuongeza ufanisi na kukuza taaluma hiyo yenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya teknolojia nchini.