Cameroon yatoa mchezaji bora AFCON 2017
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon Christian Bassogog ametangazwa kuwa mchezaji bora wa jumla wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), iliyohitimishwa usiku wa jana kwa timu hiyo ya Cameroon kutwaa ubingwa.