"Nampenda Rais Magufuli" - Bwege
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara maarufu kama 'Bwege' amefunguka na kudai katika viongozi ambao anawapenda katika nchi hii ni Rais Dkt. John Magufuli huku akimuomba asimamie haki za wananchi kwani akifanya hivyo ataweza kushinda hata miaka 100.