Mkuu wa Mkoa ainusuru Ndanda fc Singida
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ameguswa na kilio cha klabu ya Ndanda ya mkoani humo kwa kuichangia Sh 3,250,000 baada ya kukwama mkoani Singida kufuatia kukosa pesa ya kulipia gharama za malazi na safari ya kurudi.