Hatma ya Kubenea na Komu CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kesho Alhamisi kinatarajia kutoa hatma ya wabunge wake wawili Saed Kubenea wa jimbo la Ubungo pamoja na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini, Antony Komu kufuatia wabunge hao kudaiwa kupanga njama za kumdhuru moja ya mwanachama mwenzao.

