Kuchangia chama ni lazima - Mbunge CHADEMA
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Gibson Meiseyeki amekosoa madai ya aliyekuwa Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea kiongozi huyo kujiuzulu ni kuwepo kwa michango mingi ndani ya chama hicho.