Zitto afika kimataifa Sakata la CAG na Spika
Baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali kwenda kuhojiwa kwenye Kamati Maadili, Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT, Zitto Kabwe ameamua kumuandikia barua Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Akbar Khan akimtaka kuingilia kati.

