Wanafunzi UD watishia 'kuandamana', watoa saa 72
Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imetoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo (HESLB), kuhakikisha imembadilisha Afisa Mikopo chuoni hapo, kurudisha fedha zote za wanafunzi zilizokatwa pamoja na kuwapangia mikopo wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao rufaa zao zimetupiliwa mbali.