Mwanamke wa kwanza ajitokeza kuwania Urais
Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), kimesema kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu kumekuwa na mwamko zaidi kwa upande wa wanawake ndani ya chama hicho, ambapo kati ya watia nia ya Ubunge na Udiwani 160 nchi nzima zaidi ya watia nia 40 ni wanawake.

