Kubenea ataja sababu za kutokugombea Ubunge
Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA aliyemaliza muda wake Saed Kubenea, amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizopelekea yeye kutokuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya chama hicho ni pamoja na migawanyiko iliyopo ndani ya chama sanjari na yeye kusakamwa.

