Membe kuwania Urais, aahidi mazungumzo na CHADEMA
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, amekubali kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, na kwamba huo ni wakati muafaka kwake wa kushiriki mazungumzo na vyama vingine ili waweze kusimamisha mgombea mmoja.

