Jumatatu , 18th Mei , 2015

Kocha wa Timu ya Jeshi Stars inayoshiriki michuano ya wavu mkoa wa Dar es salaam, Lameck Mashindano amesema, michuano hiyo imezidi kuwa na changamoto inayochangia timu yake kushuka hadi nafasi ya pili katika Ligi hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Mashindano amesema, katika michuano hiyo, kila timu imekuwa ikihitaji kushika nafasi za juu ambapo kumekuwa na changamoto za kiushindani, suala linalochangia kila timu kijitahidi kupata pointi za juu.

Mashindano amesema, licha ya changamoto hizo zilizochangia hadi hivi sasa kuwa katika nafasi ya pili lakini anaamini bado anauwezo wa kushika nafasi ya kwanza na mwisho kuibuka na ushindi.