Jumatano , 25th Mar , 2015

Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi katika zoezi la kupambana na matumizi ya madawa ya kulevywa katika maeneo mbalimbali.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema kuongezeka kwa biashara na matumizi ya madawa ya kulevya imetokana na wananchi kutokuwa na ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi katika uthibiti wa madawa hayo.

Kamanda Mungi ameongeza kuwa watuhumiwa wa madawa ya kulevywa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani ndugu na jamaa ya watuhumiwa hao wamekuwa wakiwatoa kwa dhamana na watuhumiwa kuachiwa huru na kuendelea na matumizi ya madawa hayo.

Aidha amesema matumizi ya madawa ya kulevywa yamepelekea kuongezeka kwa vitendo vya uharifu na kuathiri afya za watumiaji hasa vijana kutokana na baadhi ya watu kutumia vipatyo vyao kwa kuendelea kujihusisha na biashara hiyo kwa kuwatumia vijana.

Hata hivyo,Kamanda Mungi uthibiti wa madawa ya kulevywa aina ya bangi umekuwa ni mgumu kutokana na kuendelea kwa uzalishaji wake hasa katika milima ya udekwa wilaya ya kilolo mkoani Iringa na mikoa jilani ya Njombe,Mbeya na Morogoro.