Jumatano , 26th Nov , 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema Jumanne kwamba anamtuma mjumbe wake Steve Witkoff kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin huko Moscow wiki ijayo, kama sehemu ya mpango wake wa kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Trump alichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba kulikuwa na "mambo machache ambayo bado hawajakubaliana" licha ya viongozi wa Ulaya kuonyesha mashaka makubwa.

Trump pia alielezea matumaini ya kukutana na Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky "hivi karibuni", lakini akitahadharisha atafanya hivyo ikiwa kutakuwa na hatua zilizopigwa kwenye makubaliano hayo.

Baadaye Trump aliwaambia waandishi wa habari akiwa kwenye ndege ya Air Force One kwamba Witkoff anaweza kuungana na mkwewe Jared Kushner huko Moscow.