Jumatano , 29th Oct , 2025

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, leo Oktoba 29, 2025, ameongoza wananchi wa mkoa huo katika zoezi la upigaji kura na kutoa wito kwa wakazi wote kuendelea kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba.

Amesema serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi wanatekeleza haki yao ya kikatiba kwa amani na utulivu, bila hofu yoyote.

Kheri James amewahimiza wananchi wa Iringa kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vyao vya kupigia kura ili kuchagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa demokrasia.

“Tunashukuru wananchi waliojitokeza mapema. Zoezi linaendelea vizuri na hali ni salama. Nawasihi wote ambao bado hawajapiga kura wajitokeze,” amesema Mkuu wa Mkoa huyo.