
Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 2.5 duniani kote watahitaji kutafutiwa makaazi mwaka ujao, katika wakati ambapo Marekani na mataifa mengine yanapunguza wahamiaji.
UNHCR imesema idadi ya wanaohitaji kupatiwa makaazi imepunguwa kiasi mwaka huu kutokana na mabadiliko ya kisiasa yaliyoshuhudiwa nchini Syria ambako raia wake wameruhusiwa kurejea kwa khiyari nchini humo.
Msemaji wa UNHCR, Shabia Mantoo amesema kuna idadi kubwa ya wakimbizi ambao huenda wakahitaji kutafutiwa nchi za kwenda kuishi mwaka 2026, kutoka Afghanistan,Syria,Sudan Kusini, Warohigya kutoka Myanmar na Wakongomani.