
Mohamed Dewji
“Tumefuzu nusu fainali baada ya kukwama kwa miaka misimu mitano mfululizo, na tumepanda viwango vya CAF kutoka nafasi ya 7 mpaka nafasi 4 kwa ubora Afrika na hayo sio malengo yetu.
Nusu fainali si malengo ya Simba SC nusu fainali ni mapito ya Simba SC, nafasi ya nne si malengo ya Simba SC nafsi ya nne ni mapito ya Simba SC tunaitamani sana nafasi ya kwanza na inawezekana ikawa ngumu kutokana na anayeishikilia Al Ahly lakini tunaweza kumsogelea kwa kukaa nafasi ya 3 na 2
Na kazi ya kuzitafuta hizo nafasi itaanza Aprili 20 dhidi ya Stellebosch” Ahmed Ally Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC