Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Bahi Omar Badwel wakati akijibu baadhi ya changamoto za wananchi.
Baduwel ametoa agizo hilo leo kwenye uzinduzi wa mnara wa kampuni ya mawasilino ya simu ya TTCL iliyofanyika katika kata hiyo ambayo ilikuwa haina mawasilino tangu nchi hii ilipopata uhuru.
Amesema ili serikali iendelee kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ni lazima ile miradi iliyopo iendelee kulindwa na kutunzwa ili idumu kwani kuna maeneo mengine ya nchi ambayo yanahitaji huduma kama hizo lakini kutokana na ufinyu wa bajeti hawapati.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya simu ya TTCL, Mhandisi Ekael Manase amesema kata ya Nondwa ni miongoni mwa kata 20 Tanzania ambazo zimepata mradi wa kufikiwa na huduma ya mawasilino ambapo hapo awali hazikuwa na huduma hiyo kabisa.
Amesema mnara uliojengwa katika Kata hiyo una uwezo wa kuhudumia vijiji vinne vya Zejele, Maganga, Chiguluka na Sanza kuwaomba wananchi wa maeneo hayo kuulinda mnara huo ili mawasiliano yaendelee kuwepo.