
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa amesisitiza kuwa ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanyika Afrika ikitarajia kuleta chachu katika maendeleo ya sekta ya utalii.
Aidha Balozi Mussa ameeleza kuwa Ziara hiyo ya kitalii itahusisha mabalozi na wawakilishi wa mashirikika ya kimataifa 84 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini huku wadau wa sekta binafsi wakitakiwa kuitumia fursa ya ziara hiyo.
Ziara hii itahamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika biashara ya Utalii sambamba na kuwafanya mabalozi kuweza kuimarisha uhusiano wao na wadau wa sekta binafisi.
Maeneo watakayotembelea ni pamoja na Ngorongoro Creater, hifadhi ya Serengeti, pamoja na Visiwa vya Zanzibar ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atafungua rasmi Ziara hiyo itakayo Tamatishwa Zanzibar na kufungwa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi.