Ijumaa , 7th Feb , 2025

Mwanadiplomasia wa Urusi amefukuzwa nchini Uingereza katika mzozo wa hivi karibuni wa kurushiana maneno baada ya Moscow kumtimua afisa wa Uingereza mwaka jana.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy alisema hatua imechukuliwa kufuatia hatua ya Urusi ya kumfukuza mwanadiplomasia wa Uingereza mnamo Novemba.

Urusi ilimshutumu mwanadiplomasia huyo kwa kutoa habari za uongo na ujasusi kama sababu za kumtaka aondoke.
Serikali ilisema Uingereza haitakubali vitisho kwa wafanyikazi wetu kwa njia hii na kwamba hatua yoyote zaidi itakayochukuliwa na Urusi itachukuliwa kama ya uhasama na itajibiwa ipasavyo".

Balozi wa Urusi nchini Uingereza Andrey Kelin, ambaye amekuwa katika wadhifa huo tangu 2019, aliitwa katika Wizara ya mambo ya nje ili kufahamishwa kuwa kibali cha mmoja wa wanadiplomasia wake kimebatilishwa.