Taifa Stars imepoteza michezo yake yote mitatu iliyocheza kwenye michuano ya Mapinduzi ya Zanzibar,hofu imetanda kutokana na Wachezaji ambao wataunda kikosi kitakachoshiriki mashindano ya CHAN wengi wao wametumika katika michuano ya Mapinduzi.
Zikiwa zimesalia siku chache mashindano ya nchi Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi za ndani Maarufu CHAN yaanze,mashindano ambayo yatafanyika kwa muunganiko wa mataifa ya Tanzania,Kenya na Uganda.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika Februari 1 mpaka 28 ambapo yatafika tamati.Wasiwasi umeanza kutanda kwa Mashabiki wa Soka Tanzania baada ya kushuhudia timu yao ikifanya vibaya katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea Visiwani Zanzibar.
Taifa Stars imepoteza michezo yake yote mitatu iliyocheza kwenye michuano ya Mapinduzi ya Zanzibar,hofu imetanda kutokana na Wachezaji ambao wataunda kikosi kitakachoshiriki mashindano ya CHAN wengi wao wametumika katika michuano ya Mapinduzi.
Ligi yetu imekuwa na kushika nafasi ya Sita Afrika lakini hakuna uhalisia wa moja kwa moja na linapokuja kwenye timu yetu ya taifa.Vilabu vya Simba,Yanga na Azam ambavyo ndivyo alama ya mpira wetu wa Tanzania vinatumia Wachezaji wa Kigeni ambao kwa kiasi kikubwa wanachangia mafanikio ya timu hizo kwenye mashindano ya Vilabu Afrika kombe la klabu bingwa na Shirikisho.
Malengo ya kufanya vizuri mashindano ya CHAN ni makubwa kutokana na kufanyika ukanda wa Afrika ya Mashariki lakini Tanzania ikiwa ni moja kati ya nchi mwenyeji.Kiwango kilichoonyeshwa na timu ya Tifa Stars kimezua maswali mengi kwa Mashabiki wake kama inaweza kufanya vizuri mashindano hayo ya mataifa ya Afrika.
Kuna somo tunalopaswa kulipata kwa matokeo ya timu ya taifa katika mashindano ya Mapinduzi na uhalisia wa mpira wetu,kuna tofauti kubwa ya viwango vya Wachezaji wetu wa ndani ukulinganisha na wale wachache wanaocheza nje ya mipaka ya Tanzania.Hivyo zinahiotajika juhudi za makusudi kuandaa Wachezaji wapya ambao wataweza kushindana kimataifa.
Timu ya Taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) imepoteza michezo yote mitatu katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea huko Gombani Zanzibar. Stars ilipigwa 2-0 dhid ya Burkina Faso hapo jana ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabovu ikiwemo michezo miwili ya awali waliochapwa 1-0 dhidi ya Zanzibar Heroes, kisha kuburuzwa 2-0 dhidi ya Kenya na kushika nafasi ya mwisho katika msimamo kati ya Timu 4 shiriki.
Kikosi cha Kilimanjaro Stars chini ya Kocha Ahmad Ally anayekinoa kikosi cha JKT Tanzania, kimeondoka matupu bila kufunga goli lolote hata la kuotea na kurusa magoli magoli 5 katika michezo hiyo. Ikumbukwe Mapinduzi Cup ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya CHAN2025 Itakayofanyika ukanda wa Afrika Mashariki Tanzania, Kenya na Uganda mapema mwezi wa Pili.