Alhamisi , 21st Nov , 2024

Wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wametakiwa kuwekeza katika viwanda Vya uongezaji thamani Madini ili nchi iweze kunufaika na rasilimali zilizopo.

Naibu spika wa baraza la wawakilishi, Mgeni Hassan

Akiongea kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, naibu spika wa baraza la wawakilishi, Mgeni Hassan kwenye hafla ya kufunga Mkutano wa kimataifa wa Madini, anasema, viwanda vitachochea nchi kufaidika na rasilimali.
“Wawekezaji wanatakiwa kuunga mkono Serikali katika kuongeza thamani Madini nchini, ili nchi inufaike ipasavyo na uwepo wa rasilimali hizo mpaka kufikia uzalishaji wa bidhaa”, Mgeni  Hassan, Naibu Spika baraza la wawakilishi.

“Ilifanyika tafiti kwenye Kisiwa cha Pemba, na kumegundulika Madini ya vifaa Vya ujenzi, simu, betri pamoja na ndege, hivyo niwakaribishe wawekezaji kukimbilia fursa hii kuwekeza kwenye visiwa hivyo”, Antony  Mavunde, Waziri wa Madini.

Baadhi ya wachimbaji wameomba Serikali kuwawezesha vifaa pamoja na mitaji ili waweze kufanikiwa.
“Wachimbaji wengi hatuna mitaji na kitu tunachojitaji hapa sio Pesa bali ni vifaa Vya uchimbaji ili tufanye uzalishaji wenye tija”, Raenatus  Kapila, Mchimbaji Madini ya Bati.

“Wachimbaji wadogo tunasbuliwa na wamiliki wa maeneo kuna muda tunashindwa kufanya uzalishaji kwa sababu wamiliki wa Ardhi wanataka zaidi ya tunachowekeza”, Kuruthum Issa, Mchimbaji Madini ya Nikel.