Ijumaa , 8th Nov , 2024

Kikosi cha Tabora United kutokea mkoani Tabora kimefanikiwa kuondoka na matokeo ya ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga SC siku ya jana uwanja wa Azam Complex Chamazi Mbagala Dar es salaam.

Kipigo cha jana kwa Wajangwani kimekuwa cha pili mfululizo baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam wiki iliyopita. Hii inakuwa mara ya kwanza Yanga SC kupoteza michezo miwili mfululizo tangu mwaka 2020.

Kikosi cha Tabora United kutokea mkoani Tabora kimefanikiwa kuondoka na matokeo ya ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga SC siku ya jana uwanja wa Azam Complex Chamazi Mbagala Dar es salaam.

Kipigo cha jana kwa Wajangwani kimekuwa cha pili mfululizo baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam wiki iliyopita. Hii inakuwa mara ya kwanza Yanga SC kupoteza michezo miwili mfululizo tangu mwaka 2020.

Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso amekosa mkwaju wa penati ambayo ingefufua matumaini ya Wanajamgwani kurejea mchezoni, penati yake ilidakwa na Golikipa wa Tabora Hussein Masalanga ambaye alisimama imara langoni mwa timu yake kabla ya kupata majereha na nafasi yake kuchukuliwa na Haroun Mandanda.

Goli mbili za Offen Chikola na moja la Nelson Munganga zilitosha kuihakikishia Tabora United ushindi wake wa tatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2025 goli la kufutia machozi la Yanga SC likiwekwa kimiani na Clement Mzize.

Dar es salaam Young Africans ilikosa huduma ya Wachezaji wake wanne muhimu wa kikosi cha kwanza Ibrahim Hamad,Dickson Job,Boka Chadrak na Kouassi Attohoula Yao anayeuguza majeraha ya kifundo cha mguu.

Aziz Andabwile alicheza nafasi ya Mlinzi kati aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Khalid Aucho,Prience Dube, Jean Ottos Baleke na Clatos Chota Chama wote walianzia benchi kwenye mchezo huo. Mchezaji Stephane Aziz Ki anagawanya Mashabiki wa Yanga SC kutokana na kuonyesha kiwango duni msimu huu.

Timu ya Yanga ambayo ndio Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania itakabailiana na Singida Big Stars Novemba 21 baada ya ligi kuu kurejea kisha kuikabili Al -Hilal mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika Novemba 26.

Miguel Gamondi raia wa Argentina ambaye anakinoa kikosi cha Wananchi amesikika mara kadhaa akilalamikia ratiba ya ligi kubana kwa Wachezaji kucheza mfululizo kunasababisha uchovu ambao hupelekea majeraha ya mara kwa mara pamoja na kushusha viwango vya wachezaji.Kinachoendelea ndani ya Yanga SC ni athari ya kukosa muda wa kupumzika.

Kikosi hiko cha mabingwa watetezi ligi Tanzania kinashika nafasi ya 2 kikiwa na alama 24 baada ya kucheza michezo 10 Watani wake wa jadi Simba SC ikisalia kilelemi msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 1 ikiwa na alama 25 kwenye michezo 10 Singida Black Stars ikishika nafasi ya 3 ikiwa na alama 22. Ligi kuu Tanzania bara kurejea Novemba 21 baada ya kupisha michezo ya kimataifa ya kufuzu AFCON 2025.