Jumatano , 16th Oct , 2024

Instagram imetambulisha feature mpya iliyopewa jina la ''Profile card'' kwa ufupi kuhusu hii profile card ni mfanano wa Business card ila hii ya Instagram iko na pande mbili, upande mmoja ni Bio yako kwa maana ya picha na maelezo kukuhusu kama ulivyoandika kwenye Bio

Alafu upande wa pili utakuwa na QR codes ambazo mtu hatokuwa na haja ya ku-share username yako badala yake ata-scan tu kupitia simu yake na itampeleka moja kwa koja kwenye instagram profile yako.

Feature hii kwa sasa inapatikana kwa watumiaji wote wa mtandao wa Instagram, kwa wale wenye Business/proffesional accounts na casual kwa maana ya watumiaji wa kawaida wa mtandao huo. Kupitia Profile Card mtumiaji wa Instagram anapata namna mpya ya kuungana na mfuasi wake au mteja kwenye mtandao huo kwa namna rahisi ya ku-scan 

Instagram wanasema ujio wa Profile Card ni matokeo ya utafiti ambao wamefanya kwa kizazi ''Z'' yaani ''Gen -Z'' 1997 - 2012 ambao wanatumia mtandao huo, kwa mujibu wa utafiti wao ulitoa matokeo ya kwamba watumiaji wengi wa mtandao huu kwenye kizazi hii wanapenda kuwa ni watu wenyewe ushawishi kwenye mtandao wao, hivyo kupitia Profile Card itakuwa rahisi kwao kuonesha wasifu wao kwa watu wapya.

Namna ya kuipata hii Profile Card: Ingia kwenye account yako, kisha utaingia kwenye profile yako utachagua share profile alafu utaona Profile Card ikiwa imejitengeneza tayari, uta-download au ku-share kama ukihitaji

Kama hupati feature hii kwa sasa ni vyema uka-update instagram yako