Dkt. Mpango ameyasema hayo wakati akizungumza kwa niaba ya Rais katika misa takatifu ya kuadhimisha miaka 25 tangu kufariki kwake iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza katika Jimbo Kuu Katoliki Mwanza na kuongozwa na mhashamu Askofu Renatus Ngwande
“Baba wa taifa aliongoza kwa ustadi sana jitihada za kuipatia Tanganyika uhuru na kuunganisha makabila Zaidi ya 120 na kutuwezesha kutumia lugha moja tu ya Kiswahili kwa ajili ya kukuza umoja wetu na hata alikuwa tayari kuchelewesha uhuru wa Tanganyika mpaka nchi nyingine ziwe huru lakini pia chini ya uongozi wake alitoa rasilimali za nchi yake klusaidia harakati za ukombozi kwa nchi nyingine. Alia asisi muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa mmoja waasisi wa umoja wa muungano wa nchi za Afrika ili kuwaunganisha waafrika.” Amesema Makamu wa rais Dkt. Philip Mipango
Makamu wa raisi ameeleza baadhi ya mambo makubwa aliyoyafanya Mwalimu Julius Nyerere baba wa taifa huku akisisitiza tunu ya Amani aliyotuachia kama taifa na namna alivyoweza hata kuwa msuluhishi wa migogoro mbalimbali iliyokuwa ikitokea katika nchi za Afrika.