Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia CHAUMMA Salum Mwalim Jana 25,2025 ameendelea na kampeni za kuomba ridhaa wananchi wa Mwandoya, Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu.
Mwalim amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha anatengeneza barabara Za lami Jimbo lote la Kisesa, pia Mwalim amesema kuwa kilimo cha Pamba ni kilimo cha muhimu sana kwani mahitaji ya Pamba ni makubwa sana hivyo ataondoa stakabadhi gharani na kurudisha mfumo wa Pamba nyuzi na Pamba mbegu yaani malipo ya awali na malipo ya pili.

