Daniel Dubois sasa anahitaji kulipiza kisasi kwa bondia Oleksandr Usyk, ambaye alimpiga Dubois kwa TKO mnamo Agosti 2023. Dubois anahitaji pambano na Bingwa huyo wa Ukraine ili kucheza pambano la ubingwa wa dunia ambalo litamuweka katika nafasi nzuri ya uzito wa juu.
Promota Frank Warren ameeleza changamoto ya kupanga pambano na Tyson Fury, akisisitiza kuwa kuna "ugumu sana" Hata hivyo, Dubois amebaki na mtazamo wa kutaka kukutana na Usyk, akionyesha hamu kubwa ya kurekebisha makosa ya zamani na kudhihirisha ubora wake katika mchezo ngumi.