Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Amesisitiza kuwa serikali kwa sasa inawekeza katika kahawa kwa kugawa miche na mbolea ya ruzuku hivyo,anatarajia kupigwa vita na wafanyabiashara kutokana na kukemea kangomba lakini hatarudi nyuma kwa maslahi ya zao hilo.
Waziri Bashe amesema hayo katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Ruvuma mara baada ya kutembelea mashamba, viwanda vya kuchakata kahawa na skimu za umwagiliaji wilayani Mbinga na Nyasa.
"Najua haya maamuzi yatakuwa na maumivu na yatakuwa na kelele, mimi kelele nimezoea, kamateni wanaonunua kahawa kwa kangomba," amesema
Amesema, anatarajia vita kubwa dhidi ya wafanyabiashara wanaonunua kahawa kwa njia ya Kangomba na hatarudi nyuma.