Jumatano , 21st Aug , 2024

Kiungo wa Manchester City Phil Foden ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka chama cha wachezaji wa kulipwa (PFA) huku Kiungo wa Chelsea Cole Palmer akishinda tuzo ya mchezaji kijana ndani ya PFA mnamo usiku wa Agosti 20-2024 nchini Uingereza.

(Phil Foden Akiwa amebeba Tuzo ya PFA 2024)

Foden mwenye umri wa miaka 24 alifunga magoli 19 kwenye michezo 35 kwenye msimu 2023-24 ndani ya Manchester City na kushinda taji la 4 mfululizo ndani ya EPL huku jumla akiwa ameshinda mataji 6 na kuwa mchezaji kinda kushinda mataji mengi ya EPl huku kwake ni tuzo ya pili baada ya kushinda tuzo ya FWA mnamo 2023-24

Hii inakuwa ni mara kwanza kwa nyota wawili kushinda tuzo kutoka nchini Uingereza tangu msimu 2009-10 ambapo nyota wawili wa Uingereza Wayne Roney wa Manchester United na James Milner wa Aston Villa kushinda tuzo ya PFA ndani ya Ligi Kuu ya England (EPL).