Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo ulianza majira ya saa tatu usiku ya julai 23,mwaka huu ambapo walianza jitahada za kuuzima pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la zima moto na uokoaji ambao walifika ili kuweza kuudhibiti moto huo.
"Muda kuanzia saa tatu na robo tukaona banda juu linafuka moshi na kuwaka moto katika juhudi zetu tukaitana wote wafanyakazi wa Msamvu tukaanza kuzima moto,baada ya kwenda kule moto ukawa umetuzidia huku wengine wakawa wanafanya jitihada za kupiga simu fire" amesema Mohamedi Ally shuhuda.
"Vibanda vya huku nje moto ulizuka bila kujua nini chanzo chake lakini wadau wa hapa Msamvu tumepemabana kuuzima moto ule na kwa bahati nzuri jeshi la Zima Moto na uokoaji waliweza kufika na kushirikiana nao na kuweza kuuzima moto" amesema Fredi Makungu shuhuda.
Akizungumzia moto huo mwenyekiti wa mtaa wa White house,Kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro ilipo stendi hiyo bwana Saidi Yasini amesema hadi sasa bado hawajajua hasara iliyosababishwa na moto huo
"Hali ya Msamvu sio nzuri kama mnavyoona mimi nilikuwa nimelala mjumbe wangu wa serikali ya mtaa akanipigia simu ghafla akaniambia kunamoto unawaka na mimi nikakurupuka nikaja hapa"amesema mwenyekiti wa mtaa wa White House Saidi Yasini
Akithibitisha kutokea moto huo Operesheni ofisa Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zima moto na uokoaji mkoa wa Morogoro(ASF)Daniel Myalla amesema kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio wamefanikiwa kuudhitibiti moto huo na kuokoa vibanda vingine 60 ili visiungue na moto huo
"Baada ya kupata taarifa ya tukio la maoto wa Msamvu jeshi la Zima moto pamoja na wapiganaji tuliweza kufika eneo la tukio na kukuta vibanda vinateketea kwa moto kwa kutumia gari mbili,aaa tulifanikiwa kuudhibiti moto huo kwa maana kwamba kunavibanda takribani nane vilikuwa vimeanza kuungua ila tumeudhibiti kwa asilimia 90" amesema Operesheni Ofisa,mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro Daniel Myalla