(Joshua Zirkzee akisaini mkataba wa kujiunga na Manchester United)
Zirkzee mwenye umri wa miaka 23 amesaini kandarasi ya miaka 5 yenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi huku anakuwa nyota wa kwanza kusajiliwa ndani ya msimu huu chini ya utawala wa mwekezaji mpya ndani ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe.
Nyota Joshua Zirkzee amefunga magoli 12 kwenye michezo 37 kwenye msimu 2023-24 ndani ya Ligi Kuu ya Italia Seria A huku amewahi kupita ndani ya klabu za Feyenoord (Uholanzi),Bayern Munich (Ujerumani),Parma (Italia) na Anderletch (Ubelgiji) huku alijumuishwa kwenye kikosi cha Uholanzi chini ya mkufunzi Ronald Koeman kilichoshiriki kwenye shindano la UEFA EURO 2024 nchini Ujerumani