(Nyota Carlos Alcaraz akiwa amebeba taji la Wimbledon 2024)
Alcaraz mwenye umri wa miaka 21 ameweka rekodi ya kuwa mchezaji kijana zaidi kushinda mataji mawili ndani ya mwaka mmoja baada ya kushinda taji la michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open 2024) pamoja na leo kushinda taji la Wimbledon 2024.
Upande mwingine,
Kichapo cha leo kimemfanya Mserbia Novak Djokovic kushindwa kuifikia rekodi ya nyota wa zamani wa Tenisi Mswizi Roger Federer ya kushinda mataji ya Wimbledon mara 8 huku upande mwingine ameshindwa kumvuka Mwanamama Margaret Court ya kufikisha mataji 25 ya tenisi ya Grand Slam iwapo kama angeshinda kwenye mchezo wa fainali wa leo.