kikosi cha Tanzania Prisons
Akifanya mahojiano maaalam na EATV,Katibu Mkuu wa Tanzania Prisons, Ajabu Kifukwe amesema wameachana na wachezaji 10 huku mpaka sasa wamesajili wachezaji 8 huku wana imani watafanya vizuri kuelekea msimu wa mashindano 2024-25
''Usajili wote ambao umefanya una tija unakwenda kufanya vizuri na kutimiza malengo ambayo tumejiwekea ''amesema Katibu.
Tanzania Prisons ambao ni mabingwa wa ligi ya Muungano mwaka 1999 wanataraji kuweka kambi ya wiki Jijini Dar es Salaam kisha kwenda kumalizia kambi yao Jijini Mbeya huku msimu uliomalizika walishika nafasi 9 wakiwa na alama 34 kwenye michezo 30 waliyocheza kwenye msimu 2023-24.