Akizungumza wakati wa kuwakabidhi bendera Waogeleaji hao,Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Abel Odena amewataka wachezaji hao kwenda kupambana ili kuhakikisha wanarudi na medali nyumbani kutoka kwenye shindano hilo.
"Nendeni mkapambane kuhakikisha mnakwenda kuipeperusha vema bendera ya Taifa kwa kupata medali nyingi za dhahabu kwani kila kitu kinawezekana, amesema Odena.
Kwa upande wake,Kocha Mkuu wa timu ya Kuogelea ya Tanzania Alexander Mwaipasi amesema shindano hilo la Taifa la Kuogelea la Kenya wanakwenda kama timu waalikwa huku timu hiyo itawakilishwa na wachezaji 4 pekee kwenye shindano hilo.