Boston wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa baada ya kuinyuka Dallas Mavericks kwa ushindi wa alama 106 kwa 99 kwenye mchezo wa 3 wa fainali na kuwafanya kuongoza 3-0 kwenye mfululizo wa miichezo 7 ya fainali.
Nyota wa Celtics Jaylen Brown amefunga alama 30 ribaundi 8 na pasi za usaidizi wa kufunga 8 huku Jayson Tatum amefunga alama 30 ribaundi 6 na pasi za usaidizi wa kufunga 5 huku Nyota wa Mavericks Kyrie Irving akifunga alama nyingi zaidi alama 35 kwenye mchezo huu lakini haikutosha kuipa ushindi Mavericks.
Boston Celtics mabingwa mara 17 wa NBA wanahitaji ushindi kwenye mchezo mmoja kati ya michezo 4 ya fainali iliyosalia ili kutwaa ubingwa wao wa kwanza tangu mwaka 2008.