Ijumaa , 2nd Feb , 2024

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo Februari 2, 2024, inatarajia kuendelea kusikiliza rufaa ya mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) aliyehukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3, 2023.

Mfungwa Maria Ngoda

Hatua hiyo inakuja baada ya Februari 01, 2024 Mahakama hiyo Chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta ilisikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Ndg Maria Ngoda Dhidi ya Jamuhuri

Akiongoza Jopo la Mawakili kwa kushirikana na Mwanasheria wa UWT kwa upande wa Mrufani, Wakili Moses Abwindile amesema waliwasilisha sababu za rufaa 14 zilizowafanya wafikie hatua hiyo ambapo miongoni mwa hoja zilizowasilishwa ni kwamba Mkata rufaa hakutendewa haki ya kupewa msaada wa kisheria hasa kutokana na hali yake ya kiuchumi ambapo inadaiwa Mahakama ilipaswa kuwasiliana na taasisi zinazotoa msaada wa kisheria ili Mkata rufaa aweze kutetewa wakati wa kesi yake.

Hoja nyingine iliyowasilishwa ni kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa je zile zilikuwa ni vipande vya nyama ya swala au laah na Wakili Moses amesema vipo vigezo vinavyoweza kutumiwa na Wataalamu wa kutofautisha nyama ambavyo katika kesi hiyo havikutimika.