Jumanne , 5th Dec , 2023

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa "hali mbaya zaidi inakaribia kujitokeza" katika Ukanda wa Gaza, na shughuli za misaada zinaweza kusitishwa.

 

 Jeshi la Israel limesema linachukua hatua kali dhidi ya Hamas na makundi mengine yenye silaha katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza

Imeamuru kuhamishwa kwa sehemu ya tano ya mji huo - na eneo hilo limeripotiwa kushuhudia mashambulizi makali zaidi usiku wa kuamkia leo.

Kiasi ya malori 100 ya misaada yaliingia Gaza katika kila siku mbili zilizopita, lakini usafirishaji wa misaada unazuiwa na mapigano.

Kampuni kuu ya mawasiliano ya eneo hilo inasema huduma zinarejea hatua kwa hatua - baada ya kukatika kwa shughuli nyingine usiku wa kuamkia leo.

Shambulio la Hamas kusini mwa Israel Oktoba 7 liliuwa watu 1,200, huku wengine 240 wakitekwa nyara.

Wizara ya afya ya Gaza imesema zaidi ya watu 15,800 wameuawa katika kampeni ya kulipiza kisasi ya Israel, wakiwemo watoto 6,000.