Jumatatu , 20th Nov , 2023

American Rapper ASAP Rocky amefunguka kuwa collabo yake bora na Rihanna ni kupata watoto tu na hakuna kikubwa zaidi hicho kwa upande wake.

Picha ya ASAP Rocky, Rihanna na watoto wawili wa kiume

"Mimi na mpenzi wangu tungeshirikiana tungekuwa kama Team. Nafikiri tumefanya kazi kubwa kiukweli collabo yetu ni kupata watoto hiko ndio kitu bora kwetu mpaka sasa na hakuna kikubwa zaidi ya hicho" amesema ASAP Rocky.

Wawili hao ASAP na Rihanna wana watoto wawili wa kiume RZA na Riot na inasemekana kwa sasa Rihanna ni mjamzito tena kwa mara ya tatu.