Jumanne , 31st Oct , 2023

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoa wa Mwanza, imesema katika uchunguzi ilioufanya kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu imebaini mapungufu katika miradi 27 yenye thamani ya zaidi ya bilioni nane.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza James Ruge

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza James Ruge, amesema ufuatiliaji ulifanyika katika miradi 35 mkoani humo katika sekta za afya, barabara, elimu na utawala ambapo mapungufu katika miradi hiyo 27 yalikuwa ni kujengwa chini ya kiwango, uchepuzi wa vifaa na kutumia vifaa duni visivyokidhi viwango.

Aidha James amesema, uchunguzi umeanzishwa kwa miradi iliyobanika kuwa na kasoro na utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.