Jumatano , 20th Jan , 2016

Wazazi na walimu wa shule za msingi katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wametishia kufunga shule tano zilizopo katika kata yao kutokana na shule hizo kukosa walimu huku walimu wakisusia fedha zilizotolewa na serikali kusaidia mfumo wa elimu bur

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandari iliyopo Mkoani Morogoro Seleman Shemsanga

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wakuu wa shule za msingi Tandari Maguluwe, bunduki , vinile, kibigili, wametupia lawama serikali kushindwa kupeleka walimu wa kutosha huku shule za mijini zikiwa na walimu zaidi ya 20 kila shulE huku wao wakiwa hawafiki hata walimu watano tu pia wakidai fedha zilizotolewa kwa ajili ya Elimu bure hazikidhi mahitaji.

Nao baadhi ya wazazi wamesema watoto wao wanahitimu darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika kutokana na mwalimu mmoja kufundisha watoto zaidi ya 400 ambapo wamesema mfumo wa elimu bure kwa wanafunzi haitakuwa na maana endapo shule hizo zitaendelea kuwa na upungufu mkubwa wa walimu.

Akijibu malalamiko hayo kwa njia ya simu Afisa elimu wilaya ya Mvomero bwana Michael Ligola amesema hana mamlaka ya kuzungumzia kero hizo bali anayetakiwa kuyajibu ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambapo jitihada za kumtafuta mkurugenzi huyo zimegonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana.