Jumatano , 6th Sep , 2023

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kupata ajali wilayani Manyoni mkoani Singida, katika barabara kuu ya Dodoma- Singida eneo la Zimamoto nje kidogo ya mji wa Manyoni, ajali ambayo imehusisha magari matatu ikiwemo basi la kampuni ya Frester lililokuwa likitokea Dar es Salaam.

Pikipiki iliyokanyagwa na lor la Tumbaku

EATV imefika katika eneo la tukio na kukuta magari hayo matatu yakiwa katika eneo hilo, ambapo mashuhuda wa ajali hiyo na kusema kuwa watu hao waliokuwa na pikipiki walikuwa nyuma ya basi huku chanzo cha awali cha ajali hiyo kila ikionesha uzembe dereva wa basi kutaka kupita lorry lilikuwa limepaki na kusababisha ajali hiyo.

Akithibisha kutokea kupokea vifo hivyo na majeruhi daktari wa zamu katika hospitali ya wilaya Manyoni amesema kuwa walipokea miili ya watu wawili wakiwa wamefariki na majeruhi mmoja ambapo amepatiwa matibabu na kuruhusiwa .