Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ACP leonard Paul akizungumzia tukio hilo amesema waethiopia hao walitokea nchini Kenya na kupita Handeni na kuingia wilayani Mvomero na walikuwa wakijiendaa kwenda Mbeya kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini kutafuta hifadhi.
Jeshi hilo pia linamshikilia dereva wa gari hiyo na wanafanya mawasilinao na idara ya uhamiaji na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
Naye dereva wa gari ndogo aina ya Prado Musa Edmund akiongea huku akionekana kuficha sura yake anayeshikiliwa kwa kusafirisha waethiopia hao amesema alimpeleka boss wake Arusha njiani wakati anarudi alikutana na waethiopia hao mbapo waliomba awasafirishe kwa makubalinao kuwa atalipwa shilingi milioni moja hadi kuwafikisha mkoani Mbeya ambapo alilipwa nusu ya gharama hizo kwa makubalino malipo mengine yangefanyika baada kuwafikisha mkoani Mbeya