Jumatatu , 23rd Feb , 2015

Watu watatu wamefariki dunia akiwemo mtoto wa miaka kumi na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari matatu katika kata ya Songwe wilaya ya Mbeya, Jijini Mbeya nchini Tanzania.

Polisi Mkoa wa Njombe Ahmed Msangi.

Akithibitisha kutoka kwa ajali hiyo kama wa Polisi Mkoa wa mbeya Ahmed Msangi amesema ajali hiyo imetokea jana jioni baada ya gari lenye namba usajili T.144 CGX aina ya Faw liliyagonga magari matatu ikiwemo Toyota Haice ambalo lilipoteza muelekeo na kutumbukia mtoni na kupelekea vifo hivyo.

Aidha Kamanda Msangi waliwataja watu hao waliofariki dunia ni mwanaume mmoja umri kati ya miaka 45 – 50, mwanamke mmoja umri kati ya miaka 65 – 70 na mtoto wa kike umri kati ya miaka 10 – 12.

Pia Kamanda Msangi aliyataja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni gari lenye namba za usajili t.144 cgx/t.569 ckc aina ya faw track lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika kuyagonga magari matatu ambayo ni T.158 BSJ aina ya Toyota pick-up likiendeshwa na Emanuel Shedafa (28) mkazi wa Mwakibete, gari T.584 DRB aina ya toyota hiace likiendeshwa na Denis Victor (27) mkazi wa Nzovwe na gari T.623 ADQ aina ya Toyota Hiace likiendeshwa na dereva asiyefahamika.

Aidha katika ajali hiyo watu 14 walijeruhiwa kati yao 13 wamelazwa hospitali teule ya Ofisi na mmoja amelazwa hospitali ya rufaa Mbeya.