Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini
Hayo ameyabainisha hayo wakati akizungumza na madereva wa bodaboda katika Kata ya Bukabwa wilayani Butiama ambapo mbali na kuwakumbusha kufuata sheria za barabarani pia aliwagawia viakisi mwanga ambavyo vitawasaidia katika kazi yao ya usafirishaji wa abiria.
"Ajali nyingi za bodaboda zimekuwa zikisababisha ulemavu wa kudumu na vifo jambo ambalo limekuwa likipoteza vijana wengi ambao ndio Taifa la kesho," amesema naibu waziri sagini.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakazungumzia suala la mwendokasi unaotumiwa na madereva hao pamoja na kupuuza alama za barabarani na kuliomba Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kuwachukulia hatua kali wale wanaokiuka sheria za barabarani.
Nao baadhi ya madereva bodaboda wakazungumzia suala la usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuomba kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani kila mara huku wakiwaomba bodaboda wenzao kufuata sheria za barabarani.