Jumatatu , 26th Mei , 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hajafurahishwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, kufuatia shambulio kubwa zaidi la anga dhidi ya Ukraine

Katika hali ambao ni nadra sana kutokea, Trump alisema: "Ni kitu gani kilichomtokea? Anaua watu wengi sana." huku akisema "Putin amekuwa mwendawazimu"

Awali, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema ukimya wa Marekani juu ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi ndio unaompa kiburi Putin, akitoa shinikizo - ikiwa ni pamoja na vikwazo vikali - dhidi ya Urusi.

Takriban watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Ukraine usiku wa kuamkia Jumapili baada ya Urusi kufanya shambulizi la ndege zisizo na rubani na makombora 367 - idadi kubwa zaidi katika usiku mmoja tangu Putin alipoanzisha uvamizi nchini humo mnamo 2022.

Alipoulizwa iwapo anafikiria kuongeza vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi, Trump alijibu: "Kabisa." Rais wa Marekani ametishia mara kwa mara kufanya hivyo kabla - lakini bado hajaweka vikwazo vyovyote dhidi ya Moscow.
Muda mfupi baadaye, Trump aliandika katika ujumbe kwenye mtandao wa Truth Social kwamba Putin "amekuwa mwendawazimu kabisa". #EastAfricaTV