
Miongoni wachezaji aliowaita ni pamoja na Antony wa Man United anayecheza kwa mkopo Real Betis.
Nje ya Antony jina jingine ni Casemiro ambaye alipigwa chini tangu 2023. Antony mwenye thamani ya pauni milioni 85 amekuwa na kiwango bora na Real Betis tangu alipojiunga na timu hiyo mwezi Januari. Winga huyo, ambaye alitemwa timu ya taifa tangu Machi 2023, ameifungia Betis mabao tisa, na kutoa asisti tano na kumfanya ahusike kwenye mabao 14 msimu huu.
Ancelotti amekuwa meneja wa kwanza katika historia ambaye si Mbrazili kuifundisha timu hiyo ya taifa wa timu ya taifa. Muitaliano huyo ameanza rasmi majukumu yake kama meneja wa Brazil Jumatatu hapo jana Jumatatu. Brazil wanashika nafasi ya 4 katika msimamo wakiwa na alama 21 huku vinara wakiwa Argentina wenye alama 31, nafasi ya pili ni Ecuador wenye alama 23 wakati Uruguay wakishika nafasi ya tatu kwa alama 21 katika msimamo wenye timu 10.